Mwaka huu utakuwa afueni serikali ikirekebisha makosa ya mwaka jana – Taifa Leo


HUU ni mwaka mpya ambao kwa kuzingatia kauli za viongozi, kwa Wakenya hautakuwa na mapya.

Kuna kila dalili kwamba hali iliyoshuhudiwa mwaka jana itaendelea mwaka huu hasa ukiukaji wa haki za kimsingi za wanyonge huku tabaka la wanasiasa wakiendelea kuungana kuwakandamiza.

Hii ilikuwa wazi katika hotuba ya kukaribisha mwaka mpya rais alipokiri kwamba maafisa wa usalama wamekuwa wakihusika na matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya wakosoaji wa serikali yake hasa vijana wanoatumia mitandao ya kijamii.

Japo nakubaliana na rais kwamba kila uhuru una mipaka yake, hakuna uhuru wa vyombo vya usalama kuhudumu nje ya Katiba.

Kwa maoni yangu, kukiri kwa kiongozi wa nchi katika hotuba ya kukaribisha mwaka kwamba maafisa wa usalama walikuwa wakihudumu nje ya Katiba licha yake kukataa kwa muda na kulaumu baadhi ya raia walioathiriwa na ukatili huu, ni kidokezo cha hali itakavyokuwa mwaka huu; kwamba hatavumilia wanaoikosoa serikali yake hata kama ni kuweka kando Katiba yote ili kuilinda serikali isianikwe kwa maovu inayotenda.

Hali kama hii itakuwa hatari zaidi Kwa raia ambao wametelekezwa na viongozi waliowapa jukumu la kuwatetea. Ni wanasiasa wachache sana watakaosimama na raia mwaka huu kwa kuwa wataogopa kuchukuliwa hatua.

Kwa kuwa ukandamizaji wa haki za kimsingi huwa na athari kwa uchumi wa nchi, itakuwa vigumu raia wa nchi hii kujikwamua kutoka kwa mazito ya mwaka jana hata kama Serikali inaahidi ardhi na mbingu.

Hakuna ufanisi wa maana ambao serikali inaweza kuletea raia wanaolia kwa kunyimwa utawala wa kisheria unaohitaji anayekosa kufikishwa kortini kwa muda uliowekwa.

Hakuna ufanisi unaoweza kupatikana wakati serikali inalazimishia raia mipango na miradi badala ya kuwashirikisha kikamilifu na kuzingatia maoni yao.

Mwaka huu unaweza tu kuwa afueni kwa raia wa nchi hii iwapo serikali itarekebisha makosa ya mwaka jana



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*