Sheria mpya kukinga wanaoshindwa kulipa mikopo ya simu – Taifa Leo


WATU waliokopa mikopo kutoka kwa taasisi ndogo za fedha wamekingwa dhidi ya unyanyasaji zikidai madeni baada ya sheria mpya kuanza kutumika Januari 1, 2025.

Marekebisho yaliyofanyiwa Sheria ya Fedha yanakataza wakopeshaji kunyanyasa, kutumia vurugu au vitisho wakati wa kudai deni.

Sheria mpya inakusudiwa kuwalinda wakopaji wa mikopo dhidi ya mbinu za unyanyasaji wakati wa kudai madeni zinazotumiwa na wakopeshaji wasiotisha dhamana.

Sheria pia inapiga marufuku unyanyasaji au udhalilishaji wa mkopaji, mdhamini au mtu yeyote wakati wa kudai deni.Bunge mwezi uliopita lilifanya marekebisho kupitia Mswada wa Sheria za Biashara (Marekebisho) wa 2024 ili kuanzisha mifumo ya kulinda wakopaji.

Sheria sasa inakataza wakopeshaji wa mikopo midogo midogo isiyokuwa na dhamana kutumia mbinu zisizo halali kukusanya deni kutoka kwa wanaoshindwa au kuchelewa kulipa.

“Biashara ya mikopo midogo isiyo na dhamana, wakati wa kudai deni la mkopo—(a) haitanyanyasa au kumdhulumu mkopaji, mdhamini au mtu yeyote kuhusiana na ulipaji wa deni; (b) hazitatishia au kutumia vurugu au njia zisizo halali katika kukusanya au kurejesha deni, au (c) kutumia lugha chafu kwa mkopaji, mdhamini au mtu yeyote zikidai deni,” kifungu kipya 53 (2) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha, kinasema.

Sheria mpya inaamuru biashara za kutoa mikopo midogo bila dhamana kuwapa wateja taarifa sahihi kuhusu masharti ya mkopo, gharama za kifedha na kudumisha usiri wa mkopaj, nai hivyo basi kukuza uwazi katika sekta hiyo.

Inakataza haswa kuwanyanyasa au kuwadhulumu wakopaji kwa matumizi ya vitishio na nguvu wakati wa kudai deni.

IMETAFSIRIWA NA BENSON MATHEKA



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*