Mpenzi wangu ni mkono birika ingawa ana pesa kama njugu – Taifa Leo


Mpenzi hajali mahitaji yangu ingawa ana pesa nyingi. Ajabu ni kwamba tukiwa maskani za starehe huwa anatumia pesa nyingi, sio kwangu tu bali kwa marafiki zake. Ananipenda kweli?

Mpenzi wako amekuonyesha wazi kuwa ni mgumu wa kutoa pesa. Hayo ni maumbile yake na usitarajie kuwa atabadilika. Akikuoa hali hiyo inaweza kuleta ugomvi kati yenu. Fanya uamuzi unaofaa. 

Niolewe kwa sababu ya mimba au nibaki shule? 

Mimi ni mwanafunzi wa shule ya upili. Mpenzi wangu amenipachika mimba na yuko tayari kunioa. Lakini wazazi wangu wamekataa, wanasisitiza nirudi shule baada ya kujifungua. Nahofia ataniacha.

Usikubali kukatiza masomo kwa sababu ya ndoa. Umekuwa shuleni kwa miaka mingi na itakuwa hasara kwako na kwa wazazi wako kuachia njiani. Fuata ushauri wa wazazi. Kama mpenzi wako hawezi kusubiri ni heri muachane. 

Mama ananikwamilia hata niolewe

Nina mpenzi na anataka kunioa. Lakini mamangu anapinga kwa sababu mimi ndiye mtoto wake wa pekee. Anaogopa kuachwa peke yake. Nifanyeje?

Hatua ya mamako inaonyeshawazi kwamba anajali maslahi yake kuliko yako. Endelea na mipango yako na umhakikishie utakuwa ukimtembelea.

Ameniacha kwa simu
Mpenzi wangu amevunja uhusiano wetu baada ya miezi mitatu tu. Alifanya hivyo kupitia simu akaniambia nimsahau. Sikutarajia hatua yake hiyo, nina maumivu makali moyoni.

Ni haki ya mtu kuchagua kupenda ama kutopenda. Mpenzi wako amekueleza wazi kwamba hakutaki na huwezi kumbadili nia. Heshimu uamuzi wake na uendelee na maisha yako.

 

 



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*