Demu atema mume kwa madai hajui kudekeza mwanamke – Taifa Leo


MWANADADA wa Ganze, Kaunti ya Kilifi, alitangazia familia ya mumewe kwamba alikuwa amechoka na ndoa akilaumu jamaa kwa kutojua maana ya mke.

Mrembo alisema alikuwa amevumilia mumewe abadilike lakini hakuonyesha dalili za kufanya hivyo na hivyo basi hangeendelea kuishi na mwanamume asiyejua maana ya mke.

“Sitaki mseme kuwa nimemkataa mwana wenu lakini hajui maana ya mke. Nasema haya ili asinisingizie mambo mengine na iwapo ninadanganya aseme,” demu alisema huku wazazi wa jamaa wakimsikiliza.

“Masuala ya wanandoa huwa ya siri na kwa hivyo nilijaribu kumsaidia kwa miaka mitatu lakini nimeshindwa na sidhani kuna mwanadada ataweza iwapo mwana wenu hatajitolea kujua maana ya mke,” demu alisema na wazee wakasema walimwelewa.



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*