Shule zahimizwa zibuni mbinu mpya za kujiletea fedha badala ya kutegemea karo – Taifa Leo


MBUNGE wa Changamwe, Bw Omar Mwinyi, amewahimiza wasimamizi wa shule kuwazia mbinu mbadala za kufadhili shughuli za shule.

Bw Mwinyi alisema hatua hiyo itasaidia kupunguza jinsi wanafunzi hufukuzwa shule kila mara wanapokosa karo, kwa vile shule huhitaji fedha.

Akiongea katika mkutano wa mashauriano wa wadau wa elimu, alisema mwelekeo huo utasaidia kuhakikisha watoto wanabaki shuleni hadi wakamilishe elimu.

“Ninaamini ni muhimu kwa shule kutafuta mbinu mbadala za kupata fedha kama vile kuchangisha fedha kijamii, usaidizi kutoka kwa wanafunzi wa zamani na pia kutafuta ushirikiano aina mbalimbali wa kuwezesha uboreshaji miundomsingi na ufadhili wa mahitaji mengine ya shule,” akasema.

Mkutano huo uliitishwa baada ya kubainika kuwa, idadi kubwa ya watoto walikuwa wanafukuzwa shuleni kwa kukosa karo na ada nyingine za ziada, hali inayoathiri matokeo yao katika mfumo mzima wa elimu.



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*