Shangazi, mke ananikimbiza kama Ferrari chumbani nahema! – Taifa Leo


Shangazi, nimeoa mwanamke mchanga na nimegundua mahitaji yake chumbani yanazidi uwezo wangu. Sielewi ni kwa nini sababu sina matatizo yoyote ya kiafya na sitaki kutumia dawa. Je, kuna vyakula vya kuchochea hamu au kuniongezea nyege?

Sina habari kuhusu chakula cha kuchochea hamu. Labda utafute ushauri wa kitaalamu hospitalini. Lakini kuna uwezekano mkubwa hali hiyo inatokana na tofauti ya umri kati yenu.

Mpenzi yuko mbali na hataki tuonane

Mpenzi wangu anafanya kazi Mombasa nami naishi Nairobi. Nilimuona mara ya mwisho miaka miwili iliyopita. Nimekuwa nikitaka tuonane lakini kila mara ananiambia ameshikwa na kazi. Ananipenda kweli?

Anakuhadaa. Haiwezekani kwamba amefanya kazi kwa miaka miwili mfululizo bila kupata likizo hata ya siku chache. Pengine amepata mwingine lakini anashindwa kukwambia.

Sijamwambia kwamba siwezi kupata watoto

Mpenzi wangu anataka kunioa. Lakini nina wasiwasi. Nimetoa mimba mara kadhaa na daktari alisema siwezi kupata mimba. Sijamwambia mpenzi wangu kuhusu hali hiyo.

Ninaamini mpenzi wako anatarajia watoto katika ndoa yenu. Utakosea kumficha hali yako. Mueleze ili aamue iwapo atakuoa kwa misingi ya mapenzi kisha mtafute watoto njia nyingine.

Nimepata SMS za uroda kati yake na babangu

Nina mpenzi na nilipanga kumuoa. Lakini nilishtuka juzi nilipokagua simu yake nikapata jumbe za kimapenzi kati yake na baba yangu! Nimechanganyikiwa, sijui nifanye nini!

Ni aibu kubwa kwa babako mzazi kunyakua mpenzi wako. Lakini huyo ni baba na huwezi kumkabili kuhusu jambo hilo. Mwambie wazi mpenzi wako kuwa umegundua siri yao kisha muachane.

 



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*