Hujambo Shangazi?
KUNA huyu binti ambaye nilikutana naye wiki mbili zilizopita. Nampenda sana hasa ikizingatiwa kwamba yeye ni shujaa sana chumbani. Lakini tatizo ni kwamba
analewa sana. Nifanyeje?
Sijambo!
Kwanza kabisa, wiki mbili ni muda mfupi sana kumfahamu mtu. Kisha, unapaswa kujua kwamba kuna mambo mengi muhimu maishani kando na ustadi wa chumbani. Sawazisha mambo haya
kisha ufanye uamuzi wake.
Leave a Reply