Wajenzi wa nyumba za bei nafuu wakimbilia bunge wakidai Sh1 bilioni – Taifa Leo


WATALAAMU wa mradi wa Rais William Ruto wa nyumba za bei nafuu wamekata rufaa kwa Bunge la Kitaifa kuhusiana na kutolipwa pesa zao za jumla ya Sh1 bilioni kwa muda wa miezi tisa.

Katika rufaa ya Novemba 27, 2024, washikadau hawa ambao wamehusishwa kama wataalamu wa usimamizi wa mradi huo, wanasema kucheleweshwa kwa malipo kutaathiri ufanisi wa programu ya nyumba.

“Kuchelewesha malipo kwa muda mrefu kumetusababishia matatizo ya kifedha na msongo wa mawazo. Hali hii ina athari mbaya kwa utekelezaji wa programu ya makazi,” wakasema kupitia ripoti.

Rufaa hiyo ya Muungano wa Wasanifu wa Majengo nchini (AAK), Asasi ya Wasoroveya nchini (IQSK) na Taasisi ya Wahandisi nchini (IEK) ilitiwa saini na Bw Karori Maina.

Washikadau hao wanataka bunge lielekeze idara ya serikali inayoshughulikia makazi na ustawi wa miji itekeleze makubalino ya mikataba na kuwalipa.

Vile vile, wanawaomba wabunge waingilie kati ili kuhakikisha kuwa malimbikizi ya malipo yote yanashughulikiwa kikamilifu bila kukawia zaidi.

Isitoshe, taasisi hizi zinarai Bunge la Kitaifa kuchunguza mgogoro baina ya maafisa wa wizara  kuhusiana na idara ya nyumba zikidai migogoro ndiyo chanzo cha masaibu yao.

“Kwa unyenyekevu, tunaomba bunge liimarisha uwajibikaji na kulainisha michakato ya usimamizi katika mpango wa nyumba za bei nafuu ili kuzuia masuala kama haya siku zijazo,” walalamishi waliwahimiza wabunge.

Imetafsiriwa na Labaan Shabaan



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*