Leo ni leo Man City ikitua Anfield kumenyana na viongozi Liverpool – Taifa Leo


BINGWA mtetezi Manchester City watakuwa ugenini leo usiku kupambana na vinara Liverpool, wakifahamu fika kwamba kichapo ugani Anfield kitawatupa nyuma alama 11 na kuzidi kukatiza matumaini yao ya kutetea taji la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu.

Kwingineko, Chelsea watakuwa nyumbani Stamford Bridge kupambana na Aston Vill wakati Everton ikiotea wenyeji Manchester United kwenye mechi itakayochezewa Old Trafford.

Manchester City ambao kufikia sasa wamefikisha pointi 23 kutokana na mechi 12 wanakabiliwa na hali ngumu kufuatia matokeo duni yanayowaandama tangu msimu huu huanze.

Mwishoni mwa wiki, vijana hao wa kocha Pep Guardiola walikaribia kumaliza kiu cha ushindi kwenye mechi ya Kombe la Klabu Bingwa ugani Etihad ambayo Feyenoord ya Uholanzi ilitoka nyuma zikibakia dakika 15 na kulazimisha sare ya 3-3.

Kwa upande mwingine, Liverpool wanaoongoza jedwalini kwa pengo la point nane wanaendelea kufurahia maisha tangu ujio wa kocha Arne Slot mapema mwezi Juni.

Mambo yamekuwa magumu kwa Guardiola ambaye kwa mara nyingine atapanga kikosi chake bila kiungo mahiri Rodri ambaye majuzi alitwaa tuzo la Mchezaji Bora Duniani la 2024 Balon d’Or.

Mhispania huyo anayeuguza jeraha la goti anatazamiwa kurejea msimu ukielekea tamati.

Kwa kipindi cha miezi mitatu bila Rodri, City imekuwa walegevu hasa katika safu ya kiungo baada ya kushiriki mechi kadhaa bila Kevin De Bruyne aliycheza dhidi ya Feyenoord baada ya kukaa nje tangu Septemba.

Kabla ya mechi yao dhidi ya Feyenoord, City wamekuwa wakifungwa angalau mabao mawili katika mechi sita zilizopita katika mashindano tofauti kwa mara ya kwanza tangu Mei 1963.

City wamekuwa wakilemea wapinzani wao kwa miaka mingi, lakini siku hizi hata wao hutuboka mara kwa mara. Bila Rodri, hata wapinzani duni wamekuwa tatizo kwao.

Katika mechi 10 bila Rodri msimu huu, City wamepoteza makombora 17, huku wapinzani wakipenya ngome yao kirahisi, huku safu yao ya ushambuliaji ikionekana kuchanganyikiwa.

Liverpool ambao kikosi chao ni imara wamepata nafasi nyingi za kuchapa mashuti ya kulenga (20) bila timu yeyote kwenye EPL msimu huu, huku wakifuatwa na Spurs wanaojivunia tisa.

Wamefungwa mabao 12 pekee msimu huu, na kushindwa mnara moja tu katika mechiu 15. Wamepata ushindi mara 17 katika mechi 19 chini ya Slot.

Udhaifu wao pekee ni kwa beki wa kushoto Andy Robertson ambaye majuzi nafasi yake ilipewa Kostas Tsimikos. Msimu huu, beki huyo amesababisha penalti mbili kutokana na makossa ya kujitakia.

 

RATIBA YA EPL LEO:
Chelsea vs Aston Villa 4:30pm)
Manchester United vs Everton (4:30pm)
Tottenham Hotspur vs Fulham (4:30pm)
Liverpool vs Manchester City (11pm)



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*