
Nimependana na mume wa mwenyewe. Nampenda kwa sababu anatosheleza mahitaji yangu kwa kila hali. Lakini tabia ya mke wake ya kumpigia simu kila tukiwa pamoja inaniudhi. Nifanye nini?
Siamini kwamba unalalamika kuhusu mke wa mtu akimpigia simu mumewe hata baada ya kuungama kwamba mpenzi wako ni mume wa mwenyewe. Kama hali hiyo inakuchukiza, achana naye utafute wako.
Mke amejifungua mtoto lakini hii sura si yangu!
Mke wangu alijifungua mtoto wetu wa pili miezi kadhaa iliyopita. Lakini nina shaka kuhusu iwapo ni wangu. Sura yake ni ya mwanamume aliyekuwa mpenzi wake. Nifanyeje?
Maelezo yako ya maana kwamba mke wako alikucheza na aliyekuwa mpenzi wake. Huenda pia huyo ni mtoto wako na hayo ndiyo maumbile yake. Uitaka unaweza kuthibitisha ukweli hospitalini.
Sijui kama mwanangu atakubali baba kambo
Nilizaa mtoto na aliyekuwa mpenzi wangu sasa amefikisha miaka 19. Nimekuwa na mshikaji kwa miaka 2 na anataka kunioa. Sijui kama mwanangu atamkubali kama baba yake.
Mwanao sasa ni mtu mzima na uamuzi wake utategemea jinsi ambavyo utamwelezea mpango wako. Pia itategemea iwapo mpenzi wako atanasa moyo wake kwa kumkubali na kumuonyesha mapenzi ya dhati ya baba.
Tuliachana si kitambo na upweke wanilemea
Nilimuacha mume wangu mwaka jana baada ya miaka 2 yenye mateso na dhuluma. Ni miezi miwili tu na nimeanza kuingiwa na upweke. Nifanyeje?
Hiyo ni kawaida kwa mtu aliyezoea maisha ya ndoa. Hata hivyo, isikufanye urudie ndoa yenye mateso kwa sababu ni hali ya muda tu. Hatimaye utazoea na utaendelea na maisha yako upya.
Leave a Reply