Sina hamu kama zamani, sijui ni uzee? – Taifa Leo


Nina mke, na watoto wetu sasa ni watu wazima. Sielewi kinachoendelea katika mwili wangu. Siku hizi ninamaliza hata miezi miwili bila kuhisi hamu ya kushiriki unyumba. Ajabu ni kuwa sina tatizo lolote kiafya. Kuna nini?

Inawezekana hali hiyo imetokana na umri wako. Jinsi umri unavyozidi, ndivyo mwanamume anavyozidi kupungukiwa upande huo. Hata hivyo, ni vyema umuone mtaalamu wa afya ya uzazi ili ujue sababu.

 

Tulitengana lakini bado tunashiriki ngoma si haba!
Nilitengana na mume wangu tukiwa na mtoto mmoja. Lakini tumeendelea kuwa wapenzi na pia ananisaidia kulea mtoto ingawa hatuishi pamoja.

Uhusiano kati yenu ni ishara kuwa bado mnapendana. Kuna matumaini makubwa kwenu kuishi tena pamoja. Unaweza kutumia nafasi hiyo na ujuzi wako wa kimapenzi kumshawishi mrudiane.

Haya mapenzi ya simu yamenichosha!
Nimependana na mwanamume fulani kwa miaka miwili sasa. Kwa muda wote huo tumekuwa tukiwasiliana kwa simu lakini amekataa tukutane. Nahitaji ushauri wako.

Inaonekana mwanamume huyo hajawa tayari kukutana nawe, labda kutokana na hali ya kutojiamini. Masuala ya mapenzi yanahitaji subira. Mpe muda.

Mpenzi alinihepa tulipomaliza shule, nitampata vipi?

Nilikuwa na mpenzi tukiwa shuleni lakini akanihepa tulipomaliza shule. Nampenda sana na sijui nitampata namna gani kwa sababu alikataa kuniambia anakoishi. Nisaidie tafadhali.

Sielewi ni kwa nini unahangaika kuhusu mtu asiye na haja nawe. Kwa kukuficha anakoishi, amekuonyesha wazi kwamba hakutaki katika maisha yake. Achana naye utafute mwingine.

 



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*