Demu amejaa kiburi kwa sababu anajiona ni mrembo – Taifa Leo


HUJAMBO shangazi? Kwa miezi mwili iliyopita, nimekuwa nikijaribu kumrushia mistari binti huyu mtaani. Yeye ni mrembo sana na amekuwa kivutio kwa akina kaka wengi. Licha ya jitihada zangu za kutaka kumnasa, amekuwa akinipuuza na hata wakati mwingine kunionyesha dharau kupitia jumbe zake. Nifanyeje?

Sijambo! Anayokuonyesha binti huyu ni ishara tosha kwamba hana haja nawe. Usijikosee heshima kwa kuendelea kumfuata mtu ambaye hana haja nawe.

 

Mume ana makalio makubwa kunizidi!

Shikamoo shangazi? Nimekuwa katika ndoa kwa miaka sita sasa na pamoja na mume wangu tumejaaliwa watoto wawili. Tangu mwanzoni, niligundua kwamba mume wangu alikuwa na makalio makubwa kuliko yangu, suala ambalo halikunisumbua. Hata hivyo, hivi majuzi nilikutana na marafiki wapya ambao baada ya kukutana na mume wangu, wamekuwa wakinikejeli kuhusiana na maumbile yake. Nifanyeje?

Marahaba! Hayo ni maumbile na hayapaswi kukukera kwani mlipooana alikuwa vivyo hivyo. Pia, koma kutawaliwa na mawazo ya watu wengine.

 

Anapuuza zote jumbe ninazomtumia!

Vipi shangazi? Kuna kaka fulani kazini ambaye nimekuwa nikimmezea mate. Mbali na kuwa mtanashati, ana pesa. Nimekuwa nikijaribu kumuonyesha nia yangu ya kutaka kuwa na uhusiano naye kwa kumtumia jumbe kadhaa za mapenzi lakini amekuwa akizipuuza. Nifanyeje?

Salama! Mtu kupuuza jumbe zako ni ishara tosha kwamba hana haja na mawasiliano baina yenu. Tumia muda huu kumtafuta akupendaye.

 

Rafiki hunipigia kwa sababu ya mambo ya ngono!

Mpendwa shangazi, nimeoa kwa miaka mitano sasa. Hata hivyo, kuna rafiki yangu wa kike kazini ambaye ana mazoea ya kunitumia picha na video za ngono kila wakati. Hivi majuzi mke wangu alikumbana na baadhi ya jumbe zetu na kusababisha vita. Nimkomesheje huyu binti?

Wewe ni mume wa mtu na si vyema kuendelea kukubali kupokea jumbe za aina hiyo kutoka kwa mwanamke mwingine. Mkanye bayana na ikiwezekana katiza kabisa mawasiliano yenu.



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*