MTU mmoja kati ya watano duniani anaugua ugonjwa unaoenezwa kingono.
Ugonjwa huo unaosababisha vidonda kwenye sehemu za siri unafahamika kama genital herpes.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), angalau watu milioni 846 walio na umri wa miaka 15-49 wanaishi na ugonjwa huu. Angalau mtu mmoja kwa kila sekunde (watu milioni 42) wanapata maambukizi haya.
WHO inasema kuwa angalau zaidi ya watu milioni 200 walio na umri wa miaka 15-49 waliugua ugonjwa huu mwaka wa 2020.
Japo kwa saa hii ugonjwa huu hauna tiba, mgonjwa haswa mwanamke mjamzito anapopata ugonjwa huu anaweza eneza kwa mtoto akijifungua.
Kuna aina mbili za herpes, ugonjwa unaosababisha virusi vya Herpes Simplex Virus (HSV), zinazojulikana kama HSV-1 na HSV-2 na zote husababisha ugonjwa wa vidonda kwenye sehemu za siri.
Kwa mujibu wa WHO, angalau watu milioni 520 walikuwa na HSV-2 mwaka wa 2020, aina ya herpes inayoenezwa wakati mtu anashiriki ngono.
Dalili za ugonjwa huu ni kuwa na vidonda kwenye mdomo, kuhisi joto jingi, maumivu kwenye kichwa na misuli na kutatizika unapoenda haja ndogo.
Leave a Reply