Wanawake huhadaa wanaume ilhali huwa hawajafikishwa kileleni – Utafiti – Taifa Leo


WANAUME huwa hawafanyi hila kwamba wamefika kilele wakati wa mahaba ikilinganishwa na wanawake, watafiti wamebaini.

Utafiti uliochapishwa kwenye jarida linaloangazia masuala ya ngono, ulisema wanawake wengi ndio hudanganya wanaume kuwa wamefika kilele wakati wa tendo la ndoa.

“Tulibaini kuwa wanawake, watu wenye jinsia mbili (huntha), na kuwa na wapenzi wengi, ni sababu ambazo zinahusishwa na tabia ya wapenzi kudanganya kuwa wamefikia kilele wakati wanaposhiriki ngono,” sehemu ya utafiti huo inaeleza.

Aidha utafiti huo uligundua watu ambao wapo kwenye uhusiano wa wazi ndio walikuwa na tabia ya kudanganya kufika kileleni. Wale ambao wapo kwenye ndoa au uhusiano wa kudumu iligunduliwa hawakuwa sana na tabia hiyo ya kuchukiza.

Vilevile waliokuwa na tabia hiyo ya ukora, ni wale ambao hawakuwa wakiridhika na uhusiano ambao wapo, hawakuwa wakiridhishwa na wapenzi wao na pia walikuwa wakisumbuliwa na msongo wa mawazo kuhusu masuala mbalimbali maishani.

Wanaume na wanawake ambao walikuwa wakishiriki hadaa hiyo hata hivyo, walikuwa na sababu tofauti baada ya kuachana na tabia hiyo.

Wanaume walisema penzi lao lilikuwa limeimarika na sasa walikuwa wakifurahia tendo la ndoa. Baadhi walisema waliachana na wapenzi wao kwa hivyo hawakuwa wakishiriki ngono kabisa.

Wanawake nao walisema hawakuona haja ya kuwahadaa wapenzi wao na wakaridhika na maisha bila kufika kilele wakati wa mapenzi.

Utafiti uliofanywa hapo awali ulionyesha kuwa kibayolojia wanawake wakati mwingine hupata ugumu wa kufikia kilele wakati wa mapenzi.

Hii ndiyo maana baadhi yao hawamakinikii suala hilo huku wanaume wanapogundua hilo, hujilaani kuwa hawajawaridhisha kitandani.

“Tunaamini kuwa ikija katika wapenzi kufika kilele wakishiriki ngono, mazungumzo ni jambo ambalo ni muhimu sana,” akasema Dkt Silvia Pavan kutoka Chuo Kikuu cha Copenhagen.



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*