BUNYALA, BUSIA
JOMBI wa hapa alimfokea jirani yake vikali akimlaumu kwa kuruhusu wageni aliokuwa amekaribisha waje kuharibu choo chake.
Kulingana na mdaku wetu,jamaa alikuwa ameandaa hafla ya kumtoa mwanawe jandoni kabla ya kuandalia wageni hao vyakula na hata vinywaji.
Walipotaka kujisaidia,wageni waliekezwa kwa jirani Jamaa akidai hakuwa amejenga choo chake.
Walilazimika kupanga foleni ili kutimiza haja zao.Hata hivyo,mwenye boma hilo alipofika, hakufurahia kitendo hicho huku akilaumu jamaa kwa kumkosea heshima.
“Nani alikupa ujasiri wa kuandaa sherehe ukijua huna choo kwako?.Afadhali ungejenga kwanza kabla ya kuwaita wageni wako!.Umenikosea heshima sana,”aliwaka jirani.
Leave a Reply