Ruto arushia Kenneth, Wa Iria minofu – Taifa Leo


RAIS William Ruto amemteua aliyekuwa mgombea urais Peter Kenneth na aliyekuwa Gavana wa Murang’a Mwangi wa Iria kuhudumu katika serikali yake.

Katika notisi jana, Rais Ruto alimteua Bw Kenneth kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Kitaifa ya Kukadiria Ubora wa Bidhaa Kenya (KEBS). Pia, alimteua Mwangi-wa-Iria kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma.

Uteuzi mwingine uliofanywa katika notisi hiyo iliyotiwa saini na Katibu Mkuu Tawala katika ofisi ya Mkuu wa Utumishi wa Umma, Arthur Osiya, ni Noor Yaror Gabow, ambaye amekabidhiwa jukumu la kusimamia Ubalozi mdogo nchini Haiti.

Katika ilani hiyo, Dkt Ruto pia alimteua Gerald Nyaoma Arita kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Kenya, Profesa Adams G.R. Oloo kama Mshauri wa Mkakati na Mawasiliano, Dkt Silvester Okumu Kasuku kama Mshauri wa Utawala.

Wengine walioteuliwa washauri ni Meja (Mstaafu) Ali Mahat Somane kama Mshauri wa Masuala ya Usalama katika Ofisi ya Masuala ya Usalama wa Kitaifa na Joe Owaka Ager kama Katibu wa Utawala.

“Uteuzi katika Ofisi ya Rais unalenga kutia nguvu washauri wa Rais na Serikali katika kutimiza majukumu ya ofisi kuu ya taifa,” inasema sehemu ya notisi hiyo.



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*