Aliyeendesha gari kwenye umati sokoni na kuua watano kushtakiwa kwa mauaji – Taifa Leo


MWANAMUME anayeshukiwa kuendesha gari katikati ya umati katika soko la Krismasi nchini Ujerumani, shambulio lililoua watu watano na kujeruhi wengine wengi anakabiliwa na mashtaka mengi ya mauaji na kujaribu kuua, polisi walisema Jumapili.

Shambulio la Ijumaa jioni katika mji wa kati wa Magdeburg lilishtua nchi na kuzua taharuki kuhusu suala tata la uhamiaji.

Mshukiwa huyo ambaye yuko kizuizini, ni daktari wa magonjwa ya akili mwenye umri wa miaka 50 kutoka Saudi Arabia aliye na historia ya kutoa maneno ya chuki dhidi ya Uislamu  na ameishi Ujerumani kwa takriban miongo miwili. Sababu ya shambulio hilo bado haijafahamika.

Kulikuwa na “vurugu ndogo” katika maandamano yaliyohudhuriwa na karibu watu 2,100 Jumamosi usiku huko Magdeburg,  polisi walisema. Waliongeza kuwa mashtaka ya uhalifu  yatafuata, lakini hawakutoa maelezo zaidi.

Waandamanaji,  baadhi wakiwa wamevalia mavazi meusi, waliinua bendera kubwa yenye neno “wahamishwe”, neno linalopendwa na wafuasi wa mrengo wenye msimamo mkali wanaotaka kufukuzwa kwa wingi kwa wahamiaji na watu wanaochukuliwa kuwa si Wajerumani .

Wakazi wengine walikusanyika kutoa heshima zao kwa wafu.

Hakimu aliamuru mshukiwa, aliyetambuliwa na vyombo vya habari vya Ujerumani kama Taleb A, kuwekwa chini ya ulinzi wa mahakama kwa tuhuma za makosa matano ya mauaji  pamoja na makosa mengi ya kujaribu kuua na kudhuru, polisi walisema katika taarifa.

Reuters haikuweza kubaini mara moja ikiwa mshukiwa alikuwa na wakili.

Waliouawa ni mvulana wa miaka tisa na wanawake wanne wenye umri wa miaka 52, 45, 75 na 67, taarifa ya polisi ilisema. Kati ya waliojeruhiwa, karibu 40 walikuwa na majeraha mabaya.

Maafisa wa serikali walisema mshambuliaji huyo alitumia sehemu za dharura za kutokea katika eneo la soko la Krismasi, ambapo aliendesha gari kwa kasi na kwenye umati wa watu, na kugonga zaidi ya watu 200 katika shambulio la dakika tatu. Alikamatwa katika eneo la tukio.

Maafisa wa Ujerumani hawajamtaja mshukiwa na ripoti za vyombo vya habari vya Ujerumani zimetoa jina lake tu kama Taleb A. kwa kuzingatia sheria za faragha za nchi hiyo..

Mshukiwa huyo alikuwa akiukosoa vikali Uislamu hapo awali na alijitokeza katika mahojiano kadhaa na vyombo vya habari mnamo 2019 akiripoti kuhusu kazi yake ya kusaidia raia wa Saudi Arabia ambao walikuwa wametema Uislamu kukimbilia Ulaya.



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*