RAIS William Ruto amepuuzilia mbali madai ya kiongozi wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka kuwa bonasi ya wakulima wa miwa imetolewa na serikali.
Dkt Ruto alimweleza Bw Musyoka kwamba serikali imekuwa ikijipanga kuboresha usimamizi wa sekta ya sukari na ndio maana wakulima waliweza kupata bonasi kutoka kwa kampuni na wala si serikali.
Rais alisema mnamo Jumatatu, alikuwa Mumias na kuahidi kwamba angefufua sekta ya sukari.
Aliongeza kuwa serikali imeanza kufufua kiwanda cha sukari cha Mumias na ndio maana iliwapa wakulima bonasi alivyoahidi mwaka jana.
Hivyo basi, alishangaa ni kwa nini baadhi ya viongozi hawakufurahishwa na hatua kubwa ambayo serikali ilipiga kufufua sekta ya sukari iliyokuwa imezama kutokana na madeni.
“Kila mkulima analipwa kila wiki na wafanyakazi wanapata mishahara yao kila mwezi na juzi tulilipa bonasi ya kwanza kwa wakulima wa miwa. Sasa nashangaa kuna viongozi wanauliza kwanini serikali inawasaidia wakulima. Je, wakulima wa miwa si Wakenya?” alishangaa Rais Ruto.
Haya yalijiri siku moja tu baada ya Bw Musyoka kumsuta Rais Ruto kuhusu bonasi ya Sh150 milioni ya miwa.
Leave a Reply