Demu asuta baba wa kambo kwa kukataa posa kutoka kwa mpenziwe – Taifa Leo


KIPUSA wa hapa alizua kisanga akimlaumu baba wa kambo kwa kukataa posa kutoka kwa mpenzi wake.

Duru zinasema kuwa demu alimleta jamaa nyumbani na wazazi wake wakamkaribisha kwa mikono miwili.

Kisanga kilitokea baba wa kambo alipodinda kupokea posa akisema ilikuwa kidogo ishara kwamba jamaa alidharau familia yake.

“Unajua umuhimu wa ndoa kweli? Rudi na posa yako duni. Huna heshima hata kidogo,” baba wa kambo alisema na kuwataka wawili hao watengane.

Hata hivyo, binti alisimama kidete na kuapa hatatengana na mpenzi wake.

“Kama mpango wako ni kuharibu uhusiano wetu utasubiri sana. Siwezi kutengana na mpenzi wangu ng’o! Kama hutaki posa hakuna mtu wa kukulazimisha,” binti alisema.

Inaarifiwa kuwa demu na jamaa waliondoka baada ya tukio hilo.

 



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*