Eldoret bado yapambana kutimiza masharti ya jiji – Taifa Leo


USIMAMIZI wa Eldoret unapambana kutimiza masharti ya viwango yaliyosalia, miezi minne baada ya Rais William Ruto kuupandisha hadhi kuwa jiji.

Miongoni mwa masharti hayo ya lazima ni kuanzishwa kwa jumba la ukumbusho la kitaifa ambalo usimamizi wa jiji unajenga katika shamba la Huduma ya Misitu ya Kenya (KFS) kando ya barabara kuu ya Eldoret-Iten.

Rais Ruto, mnamo Agosti 15, alipandisha hadhi ya mji wa Eldoret kuwa jiji kujiunga na Nairobi, Mombasa, Kisumu na Nakuru.

Ukiwa na takriban watu 500,000, Eldoret imeorodheshwa mji unaokua kwa kasi zaidi kwa sasa nchini na unatumika kuunganisha nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Shughuli nyingine iliyosalia ni pamoja na utekelezaji wa Mpango wa Usimamizi wa trafiki kati kati mwa jiji, uwekaji lami njia za watembeao kwa miguu, kuhamisha wafanyabiashara wa Jua Kali hadi maeneo yaliyotengwa miongoni mwa mengine.

Masharti mengine ambayo hayajashughulikiwa ni pamoja na wajibu wa wamiliki wa majengo kupaka majengo rangi moja isiyohusishwa na chapa yoyote ya kibiashara au wakabiliwe na faini au kifungo cha miezi sita na kutwaa tena ploti ambazo wamiliki hawajaziendeleza.



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*