Genge liliua watu 207 Haiti kwa tuhuma za uchawi, Umoja wa Mataifa wasema – Taifa Leo


TAKRIBAN watu 207 waliuawa mapema Desemba  na wanachama wa genge la Wharf Jeremie katika mji ulio bandarini wa Cite Soleil nchini Haiti, Umoja wa Mataifa ulisema katika ripoti uliotoa Jumatatu, ikirekebisha ya awali iliyosema watu  kuwa 187 waliuawa.

Kenya imetuma polisi wapatao 400 katika nchi hiyo kudumisha amani.

Katika ripoti yake mpya kuhusu mauaji hayo, Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa ilisema takriban wanaume 134 na wanawake 73, wengi wao wakiwa wakazi wazee waliotuhumiwa kwa uchawi, waliuawa katika kipindi kisichozidi wiki moja cha mauaji ya halaiki na utekaji nyara walipovamiwa na wanachama wapatao 300 wa genge la Wharf Jeremie.

Kiongozi wa genge hilo Monel “Mikano” Felix aliamuru mashambulizi hayo baada ya mtoto wake kuugua, akiwashutumu wakazi wa eneo hilo kwa kusababisha ugonjwa huo kupitia juju. Wengi wa wahasiriwa walitekwa nyara kutoka kwa mahekalu wakati wa sherehe za kidini, Umoja wa Mataifa ulisema.

Mauaji hayo yalishtua taifa  hilo , ambalo limekumbwa na mzozo mbaya wa magenge, na kusababisha uhaba mkubwa wa chakula, huku majirani zake wakichelewa kutoa msaada wa usalama ulioahidiwa kwa muda mrefu.

Genge la Mikano limedhibiti eneo dogo lakini la kimkakati kati ya bandari muhimu, ghala zinazozunguka na barabara kuu za kitaifa nje ya mji mkuu kwa miaka 15, kulingana na Umoja  wa Mataifa.

Baada ya mauaji hayo wanachama wa genge hilo walijaribu kufuta ushahidi kwa kukamata simu za mkononi, kuchoma miili na kuitupa baharini.

Zaidi ya watu 5,300 wameuawa nchini Haiti tangu Januari na zaidi ya 12,000 tangu kuanza kwa machafuko ya magenge  2022, kulingana na Umoja wa Mataifa huku zaidi ya 700,000 wakiwa wakimbizi wa ndani.

 

 



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*