Hussein abwaga Team Nick Mwendwa kuchaguliwa rais mpya wa soka FKF – Taifa Leo


HUSSEIN Mohammed alikuwa mbioni kutwaa urais wa Shirikisho la Soka Nchini (FKF) baada ya kuibuka kifua mbele katika raundi ya kwanza na kumfanya mpizani wa karibu Doris Petra kuinua mikono, katika ukumbi wa Kasarani jijini Nairobi, Jumapili.

Kwenye duru ya kwanza, Mohamed alizoa kura 43 huku mpinzani wa karibu Doris Petra akipata 31. Mohammed kisha akazoa kura 67 kwenye raundi ya pili Jumapili usiku.

Petra alikuwa akiunga mkono na Rais wa sasa wa FKF, Nick Mwendwa, ambaye pia alikuwa mgombeaji mwenza wake.

Mgombea urais Doris Petra (kulia) na mgombea mwenza Nick Mwendwa wakiwasili kuwasilisha karatasi zao za uwaniaji awali Oktoba 14. PICHA | CHRIS OMOLLO

Katika duru hiyo ya kwanza ya uchaguzi, aliyekuwa Katubu wa FKF, Barry Otieno, alipata kura 10. Cleophas Shimanyula alipata kura nne huku jagina wa Sammy Owino Kempes akipata kura mbili. Tom Alila alipata kura moja huku Chris Amimo na Katibu wa Gor Sam Ochola wakikosa kupata kura zozote.

Kwenye duru ya pili ya uchaguzi Mohamed alipata kura 67 huku Petra ambaye alikuwa amejiondoa akipata kura moja naye Otieno pia akipata kura moja.

Mwenyekiti wa klabu ya AFC, Dan Shikanda, akipiga kura katika uchaguzi huo. PICHA | CHRIS OMOLLO

Kwa mujibu wa sheria za FKF mshindi lazima angepata asilimia 50 ambazo ni kura 45 kati ya wajumbe ambao walipiga kura. Awali wawaniaji ambao walikuwa wakiegemea mrengo wa Mohamed nao walitwaa viti sita kati nane vya wawakilishi wa kwenye Baraza Kuu la FKF (NEC).

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi na Bodi ya Uchaguzi inayoongozwa na Hesbon Owila, Hussein aliahidi kuyatekeleza yote yaliyokuwa kwenye manifesto yake huku akichukua rasmi usukani katika jumba la Kandanda, Kasarani.

“Imekuwa safari ya kipindi kirefu na sasa imani ambao wajumbe wameonyesha kwa kunipa uongozi wa FKF nitaitumia kutimiza yale yote ambayo niliyaahidi,” akasema Mohamed.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi na Bodi ya Uchaguzi inayoongozwa na Hesbon Owila, Mohammed aliahidi kutekeleza yote yaliyokuwa kwenye manifesto yake huku akichukua rasmi usukani katika jumba la Kandanda, Kasarani.

“Imekuwa safari ya kipindi kirefu na sasa imani ambao wajumbe wameonyesha kwa kunipa uongozi wa FKF nitaitumia kutimiza yale yote ambayo niliyaahidi,” akasema Mohamed.

Mohammed (kushoto) na mgombea mwenza McDonald Mariga walipozindua kampeni yao mjini Nairobi mwezi Oktoba. PICHA | CHRIS OMOLLO

Wajumbe hao 90 walioshiriki uchaguzi walijumuisha wenyekiti 46 wa FKF kaunti, 18 wa Ligi Kuu ya Soka (KPL), 10 wa Ligi ya Kitaifa ya Supa (NSL) na 10 wa Ligi ya Kitaifa ya Daraja ya Kwanza wanaume. Wengine ni watatu wa Ligi ya Wanawake (KWPL), wawili wa NSL wadada na mmoja chama cha maslahi ya wachezaji.



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*