Jamaa ahepa na pesa za matanga alizopewa na mwanasiasa Bomet – Taifa Leo


POLO aliyepokezwa hela za mazishi na mwanasiasa hapa Chepalungu, Kaunti ya Bomet, alihepa nazo akisema zilikuwa zake.

Duru zinaarifu kuwa polo ni mfuasi sugu wa kigogo huyo wa siasa.

Juzi familia yake ilipopata msiba polo alimwalika mwanasiasa huyo kutoa mchango wake ili kumsindikiza mwendazake.

Siku yenyewe kigogo huyo alimpa jamaa bahasha nzito baada ya kuhutubia kusanyiko, lakini polo alitia mfukoni mara moja.

Kamati ya mazishi ililete pesa hizo mezani ili zisaidie kugharimia mahitaji mazishini, kalameni alishikilia kwamba zilikuwa zake eti kwa sababu mwanasiasa huyo alikuja kupitia mwaliko wake.

“Unataka kufaidi kutokana na kifo cha jamaa yako! Wewe namna gani. Ni laana kubwa kufanya hivyo!” polo alisutwa na wanakamati lakini alikaa ngumu hakubadilisha msimamo.



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*