WANAWAKE watatu wameaga dunia baada ya kula keki ya kusherehekea sikukuu ya Krismasi katika kinachoshukiwa kuwa kisa cha kutiliwa sumu.
Jamaa watano wa familia moja, wanawake wanne na mtoto mmoja, walianza kuugua na kupelekwa hospitalini baada ya kula keki usiku wa kuamkia sikukuu ya Krismasi 2024, Jumatano, Desemba 25, mjini Torres, jimbo la Rio Grande do Sul, zilisema ripoti.
Wanawake watatu walipoteza maisha yao huku wa nne, aliyeandaa keki hiyo, pamoja na mpwa wake mwenye umri wa miaka 10, wangali wanatibiwa.
Hospitali ya Nossa Senhora dos Navegantes inayowahudumia ilieleza vyombo vya habari Jumamosi kuwa hali yao inaonekana kuimarika.
Wapelelezi waligundua kemikali yenye sumu kwa jina arsenic kwenye damu ya jamaa watatu wa familia lakini haikubainisha ikiwa watatu hao ndio waliofariki.
Imetafsiriwa na Mary Wangari
Leave a Reply