Kiswahili kati ya masomo watahiniwa waliona ‘giza’ – Taifa Leo


SOMO la Kiswahili ni miongoni mwa masomo 10 ambayo matokeo yalishuka kulingana na matokeo ya KCSE, ya 2024, yaliyotolewa Alhamisi, Januari 9, 2024.

Kulingana na Waziri wa Elimu Julius Migos Ogamba, masomo mengine yaliyoandikisha matokeo duni ikilinganishwa na mwaka wa 2023, ni; lugha ya Kiingereza, Bayolojia kwa vipofu, Somo la Kidini ya Kikristo, Sayansi Kimu, Ujenzi, Somo la Masuala ya Umeme, Muziki, Masomo ya Lugha za Kifaransa na Kijerumani na Muziki.

Hata hivyo, watahiniwa wa KCSE 2024 waliandikisha matokeo bora katika masomo 17 ikilinganishwa na matokeo ya 2023.

Masomo hayo ni pamoja na Hisabati, Bayolojia, Fizikia, Kemia, Sayansi jumla, Historia na Serikali, Jiografia, Dini ya Kiislamu, Kilimo, Useremala na Utengeneza Vitu vya Chuma.

Masomo mengine ni Uchoraji, Teknolojia ya Usafiri wa Angani, Somo la Kompyuta, Lugha ya Ishara ya Kenya na Somo la Biashara.

 



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*