Korti yazuia seremala aliyepatwa amebeba viungo vya mwili wa mkewe kwenye begi – Taifa Leo


SEREMALA anayeshukiwa kuua mkewe mwenye umri wa miaka 19 na kukatakata mwili wake kisha akapakia vipande kwenye begi atasalia rumande kwa siku 21 ili kuwezesha maafisa wa polisi kukamilisha uchunguzi.

Hakimu mkuu mwandamizi wa mahakama ya Milimani Gilbert Shikwe aliamuru John Kyama Wambua, 29 kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Ruaraka kwa muda wa siku 21 kwa mauaji ya Joy Fridah Munani.

John Kyama Wambua, 29, aliyepatikana amebeba viungo vya mwili wa mkewe kwenye begi, katika picha hii akiwa kortini, Jumatano. Picha|Richard Munguti

Mahakama ilisema kuwa visa vya mauaji ya wanawake vinaongezeka na polisi wanahitaji muda wa kuchunguza kwa kina kesi hiyo.

Wambua anashukiwa kumuua mkewe Januari 20, 2025, katika eneo la Kasonova, Starehe Kaunti ya Nairobi.

Kulingana na maafisa wa uchunguzi wa uhalifu (DCI), Wambua alisema kuwa alimfumania mkewe akiwa na mwanamume mwingine na wakamkabili jambo ambalo lilisababisha mabishano akamuua na kuukata mwili wake vipande vipande akilenga kwenda kuutupa.



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*