Mama afokea mumewe kwa kuwa dume pekee katika chama cha akina dada – Taifa Leo


MWANADADA aliingiwa na tumbojoto alipogundua mumewe ni mwanamume pekee katika chama cha vipusa mjini Awasi, Kisumu.

Inasemekana mwanadada huyo aliolewa mwaka jana na hivyo bado anaendelea kumjua mumewe.

Juzi alishangaa kujua bwanake hutoka katika mikutano ya chama na warembo kila mara.

“Kwa nini ungurume peke yako katika chama kinachotawaliwa na wanawake? Si uache wafanye mambo yao peke yao? Kazi yako ni nini huko?” mkewe alimdadisi.

Akatoa pendekezo kwamba jamaa amwachie nafasi yake kwenye chama hicho, lakini polo hakutaka kubanduka.

“Nitachunguza zaidi kile wewe kama jogoo unafanya katika kikao cha warembo tupu,” mwanadada alimzushia polo.



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*