Mbunge ashtakiwa kwa kumjeruhi mtoto wa gavana – Taifa Leo


MBUNGE wa Turkana Kusini John Namoit Ariko pamoja na waliokuwa madiwani wawili wa Bunge la Kaunti ya Turkana wameshtakiwa kwa kumpiga mwanawe Gavana wa Turkana Jeremiah Lomurukai.

Mbunge huyo ni miongoni mwa watu tisa waliofikishwa katika Mahakama ya Eldoret kutokana na kosa hilo pamoja na kughushi nyaraka kati ya mashtaka mengine saba. Vile vile, washukiwa hao wameshutumiwa kwa kula njama za kukwepa mkono wa sheria na haki.

Kikosi cha maafisa wa uchunguzi kutoka Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai kutoka afisi za eneo la Rift Valley wakiongozwa na Inspekta Mkuu, Margret Awino Ong’ale wamekuwa wakichunguza kisa hicho tangu Mei.

Kesi hiyo ilihamishiwa Eldoret kwa sababu za kiusalama kutokana na tofauti za kisiasa kati ya viongozi hao.

Washtakiwa wengine ni pamoja na aliyekuwa Diwani Peter Lokutuni, wanablogu Davis Lopoyo na Jamostar Silale na mwanasiasa Bonfestars Ekal.

Wengine ni Joseph Elikipan, pasta wa kanisa moja mjini Lodwar, Peter Kodet (askari wa kaunti ya Turkana) na Sammy Esinyen alias Whensonko (meneja wa mbunge waTurkana Kusini).

Shtaka lililopendekezwa linasema kuwa mnamo Aprili 29, mshtakiwa alimshambulia Nimrod Ekamais Lomurukai, 16, na hivyo kumsababishia madhara kinyume na kifungu cha 251 cha kanuni ya adhabu.

Pia watashtakiwa kwa kula njama ya kushindwa haki, kumiliki mali ya wizi na kughushi nyaraka.

Kabla ya kukamatwa kwa washukiwa kulikuwa na hali ya taharuki katika Kaunti ya Turkana.

Hii ni kwa sababu ilidaiwa kuwa baadhi ya washukiwa walidhibiti utekaji nyara kabla ya kukamatwa katika maficho yao na maafisa wa upelelezi kutoka DCI.



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*