MFALME wa Uholanzi Willem-Alexander na mkewe Malkia Maxima wameratibiwa kuzuru Kenya kwa mwaliko wa Rais William Ruto.
Ziara ya Mfalme huyu nchini ni ya pili kwa kiongozi wa hadhi hiyo kutembelea Kenya tangu Dkt Ruto alipoingia mamlakani. Mfalme Charles III wa Uingereza ndiye wa kwanza kuzuru Kenya chini ya utawala, kati ya Oktoba 31 hadi Novemba 3, 2023.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Serikali ya Uholanzi, Mfalme Willem-Alexander atazuru Kenya kuanzia Jumanne Machi 18 hadi Alhamisi Machi 20 mwaka huu, 2025.
“Ziara hii ya kwanza rasmi ya Mfalme Willem-Alexander ni kilelezo cha uhusiano mzuri na thabiti kati ya nchi zetu mbili,” ikasema taarifa hiyo iliyotolewa Jumanne, Januari 7, 2024.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa Uhalonzi unalenga kutia saini ushirikiano katika nyanja mbalimbali “huku ikiimarisha uhusiano uliopo sasa kati ya nchi hizo mbili, ikizingatiwa kuwa wajibu mkubwa wa Kenya katika mida ya kimataifa.”
“Vile vile, Uholanza na Kenya zinadumisha uhusiano wa karibu wa kiuchumi na nchini hizi mbili ni vituo vya vikuu vya kibiashara katika maeneo yao,” serikali ya Uholanzi ikaeleza.
Miongoni mwa mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa (UN) na mashirika mengine ya kimataifa, Kenya na Uholanzi zimekuwa zikifanyakazi pamoja katika masuala ya kuendeleza demokrasia, utawala wa kisheria na uhuru wa Idara ya Mahakama.
Nchi hizi mbili pia hushirikiana katika mipango ya kukabiliana na changamoto zinazohusiana na amani na usalama, mabadiliko ya tabia nchi na mipango ya utoshelevu wa chakula.
Leave a Reply