NAIBU Rais Kithure Kindiki amekanusha mada y wakosoaji wake kwamba ni mtu wa kutumia akisema yeye si mtu anayechukua msimamo binafsi.
Naibu Rais alisisitiza kuwa msaidizi mkuu wa rais hakuhitaji kukubaliana na kila anachoambiwa na bosi wake.
Kindiki alisema jukumu lake hilo halimaanishi pia kumpinga Rais kwa sababu si miongoni mwa majukumu yake ya kikatiba.
Aliongeza kuwa ingawa jukumu lake ni pamoja na kumshauri Rais, anaweza tu kufanya hivyo ikiwa Ruto atatafuta ushauri wake. Profesa Kindiki aliongeza kuwa utiifu wake ni kwa kiapo alichokula alipokuwa akiapishwa kushikilia wadhifa huo.
“Mimi ni mtu kufanya maamuzi mwenyewe. Uelewa wangu wa wadhifa wa Naibu Rais sio kumpinga Rais. Haipo kwenye Katiba, haipo katika sheria yoyote. Kuhusu iwapo Naibu Rais anaweza kumshauri Rais, jibu ni ndiyo. Kiapo nilichokula ni kumshauri Rais anapotafuta ushauri wangu na Kufanya hivyo kwa uaminifu. Haimaanishi ni lazima niufanye hadharani. Utiifu wangu uko katika kiapo cha afisi,” Kindiki alisema Alhamisi.
Kindiki alikuwa akijibu swali iwapo Rais William Ruto alimteua kuwa naibu wake kwa sababu yeye nii mtu kukubali kila kitu.
Rais William Ruto alimteua Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais kufuatia kuondolewa kwa Rigathi Gachagua.
Ruto aliangazia sababu kadha za kumchagua Kindiki kama Naibu Rais wake.
Alimtaja Naibu Rais mpya kuwa mtumishi wa umma asiyechoka katika uongozi wa kitaifa.
Ruto alisema Kindiki ni mzalendo ambaye kujitolea kwake kwa uwiano, umoja wa kitaifa na ushirikishaji hauna doa.
Kindiki aliapishwa kama Naibu Rais wa tatu wa Kenya chini ya Katiba mpya.
Kabla ya uteuzi wake, Kindiki alikuwa Waziri wa Masuala ya Ndani na Utawala wa Kitaifa.
Leave a Reply