MOTO mkubwa uliozuka umechoma sehemu ya jengo la Gandhi Wing katika Chuo Kikuu cha Nairobi.
Jengo hilo ambalo linatambuliwa mno na ambalo lina afisi za wahadhiri, vyumba vya masomo na afisi zingine nyingi za usimamizi wa kimasomo liligubikwa na moto mkali ambao ulionekana hata kwa umbali.
Muda mfupi baadaye, zimamoto waliwasili na video za wapita njia zilionyesha zimamoto hao wakipambana kudhibiti miale mikali.
Afisa wa mawasiliano John Orindi amethibitisha kufikia wakati wa kuandika taarifa hii kwamba moto huo umedhibitiwa ingawa chanzo bado hakijabainika.
Leave a Reply