MHUDUMU wa kilabu moja mjini Nyeri alikasirika nusra aache kazi baada ya kidosho mteja kumlowesha kwa pombe akidai ni mchafu.
Inasemekana kuwa shughuli za kawaida katika baa hiyo zilikuwa zinaendelea kipusa mrembo alipoingia kwa madaha na kisha akaketi.
Mhudumu alienda kumuuliza alichotaka na kipusa akaagiza chupa kadhaa za pombe.
Hata hivyo, kipusa alikunja uso kwa dharau na kudai demu aliyemhudumia alikuwa mchafu.
Weita huyo mwanadada alimpuuza na kuendelea na shughuli zake.
Kumbe pepo zitampanda kipusa kwani aliteremsha pombe yake kisha iliyobaki akamwagia mhudumu huyo na kwenda zake baada ya kulipa bili yake.
Weita huyo alipandwa na mori akaapa kuacha kazi lakini alitulizwa na wenzake kwamba ampuuze demu huyo aliyeonekana mwenye kiburi.
Leave a Reply