Mwalimu ajiondoa kufunza kwaya ya Krismasi kufuatia madai ya ufisi – Taifa Leo


POLO aliyekuwa akifunza kwaya ya akina mama katika eneo la Kipsongo mjini Kitale aliamua kupiga breki shughuli hiyo kwa hasira baada ya kusikia madai kwamba anawamezea mate.

Kulingana na mdokezi wetu,jamaa huyo alikuwa amepewa jukumu la kuwafunza kinamama hao nyimbo za sherehe ya Krismasi.

Lakini licha ya kuchapa kazi kwa uadilifu, alishtuka kupata fununu kwamba anawanyemelea waimbaji hao wa kike.

Udaku huo ulienea kote kanisani hadi kwa mchungaji, jambo lililomkasirisha polo akaamua kupiga breki kazi hiyo.

Alidai kuwa ni dharau kubwa kwa kanisa kumchafulia jina eti anamezea mate wanakwaya hao na kuambia wachungaji watafute mwalimu mwingine.



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*