Mwanadada apapura mume kwa kutumbukia mtaroni akiwa mlevi chakari – Taifa Leo


SINEMA ya bure ilishuhudiwa katika eneo la Arimi mjini Elburgon, Kaunti ya Nakuru, mwanadada alipoangushia mumewe makofi kwa kulala ndani ya mtaro akiwa amelewa kupindukia.

Inasemekana mke wa polo alikuwa amemuonya dhidi ya kutembea na marafiki wapenda pombe, ila akatia nta kwenye masikio.

Jioni ya kisanga, mwanadada alipokea simu akifahamishwa kuwa mumewe ametumbukia ndani ya mtaro na kukwama humo asiweze kujitoa.

Hapo ndipo mwanadada alifika huku anafukuta hasira kama kifaru na kuanza kumtandika jombi.

“Mara ngapi nimekuonya kwamba hawa marafiki zako watakuingiza kwenye balaa? Nyanyuka upesi kabla sijakuharibu sura,” alifokea vikali huku akimrushia makofi kadha.



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*