Mwanadada weita aliyetilia wateja ‘mchele’ kwa vinywaji atimuliwa kazini – Taifa Leo


MWANADADA aliyekuwa akihudumu katika baa ya hapa alipigwa kalamu teketeke kufuatia madai

kwamba amekuwa akiwatilia wanaume ‘mchele’ katika vinywaji vyao.

Meneja wa baa alisema kwamba alichukua hatua hiyo kufuatia malalamishi mengi kuhusu demu huyo.

Inadaiwa kidosho alikuwa akitilia wateja chembechembe za dawa hiyo ya kufanya mtu zuzu katika

vinywaji vyao kabla kuwapora hela.

Wateja walioathiriwa waliamua kuripoti kwa usimamizi kuhusu visa hivyo ili uchunguzi ufanywe.

Baada ya uchunguzi, meneja wa baa aliamuru kidosho huyo aondoke mara moja akidai amewaletea sifa mbaya na kufanya wateja wahamie kwingine.

Demu aliinuliwa juujuu na kufurushwa kama mbwa.

 



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*