Nusra vipusa maweita wamwage unga wakipigania buda mwenye fulusi – Taifa Leo


KIOJA kilizuka katika baa moja mtaani hapa vipusa wahudumu walipotiana kucha wakizozania buda aliyeingia humo kupata dozi.

Duru zinasema kuwa buda huyo ni tajiri kupindukia na vidosho walipomuona walianza kummezea maze kila mmoja akitaka kumhudumia.

Ni katika harakati zao hizo ambapo walirukiana na kurushiana matusi kabla kuanza kupigana.

“Mbona wewe unapenda kujipendekeza kwa watu. Kama hupendeki kaa mbali ama nikuharibu sura,” mwanadada mmoja alimfokea mwenzake akinyaka nywele zake nusura azing’oe kichwani.

Purukushani ilichacha akina dada hao waliporushiana makonde huku kila mmoja akimlaumu mwenzake. Buda alishangaa na kuondoka akaenda zake kusaka kinywaji baa nyingine.



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*