Papa Francis apatikana tena na tatizo la figo hali yake ikiendelea kuwa mbaya


ROME, Italia

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis anaendelea kupumzika hospitalini jijini Rome ambako amesalia kwa siku 10 akiugua maradhi ya mapafu, maambukizi tata na sasa ana shida ya figo iliyofanya hali yake kuwa mbaya zaidi.

Kwenye taarifa asubuhi, Vatican ilisema “usiku ulikuwa mzuri, Papa alilala na sasa anapumzika.”

Hata hivyo, Vatican haikutoa maelezo zaidi kuhusu afya ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki mwenye umri wa miaka 88.

Maafisa walitarajiwa kutoa maelezo zaidi kuhusu hali yake Jumatatu jioni, siku moja baada ya Vatican kufichua kuwa anakuwa na “tatizo la awali la kufeli kwa figo.”

Wakati huu, tatizo la figo “limedhibitiwa”, Vatican ikasema.

“Hajapatwa na tatizo la kupumua kama ilivyokuwa Jumamosi,” taarifa hiyo ikaongeza.

“Papa Francis alionekana kurejelewa na hisia na vipimo vilionyesha kuwa hakuwa na shida ya ukosefu wa damu baada ya kuongezewa damu mara kadhaa,” Vatican ikasema, ikiongeza kuwa Papa Francis bado alikuwa akiongezewa hewa ya ziada ya oksijeni.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki, ambaye aliwahi kutolewa sehemu mapafu alipokuwa na umri mdogo, amekumbwa na matatizo kadhaa ya kiafya katika miaka ya hivi karibuni.

Hata hivyo, mwaka huu ndio amelazwa hospitalini mwa muda mrefu zaidi baada ya kupatwa na maambukizi ya mapafu.

Sergio Alfieri, daktari wa upasuaji ambaye ni miongoni mwa wanaomhudumia Papa, alisema Ijumaa kwamba kiongozi huyo alimwambia kwamba ni mnyonge na kwamba “milango yote miwili imefunguliwa.”

Kadinali Timothy Dolan, katika mahubiri yake Jumapili katika Kanisa la St Patrick, jijini New York Amerika, alisema Papa Francis alikuwa “katika hali mbaya zaidi kiafya na kabla karibu kufa,” huku akitoa wito kwa waumini kuendelea kumwombea kiongozi huyo.

Waumini wengine wa Kanisa Katoliki kote dunia waliokusanyika kwa ibada ya Jumapili kote duniani walimwombea Papa Francis, anayeongoza Kanisa hilo lenye karibu waumini 1.4 bilioni.

Kuanzia karibu na Hospitali ya Policlinico Agostino Gemelli jijini Rome, ambako Papa huyo anatibiwa hadi Korea Kusini, hadi nchini mwake alikozaliwa Argentina, waumini walikesha wakimwombea kwa kuwasha mishumaa.

Askofu Mkuu Rino Fisichella, ambaye ni afisa wa cheo cha juu Vatican, aliwaambia waumini waliohudhuria ibada katika Kanisa la St Peter’s Jumapili kwamba wanafaa “kuhakikisha kuwa maombi yao kwa Papa ni mazito zaidi.”

Francis alichaguliwa katika wadhifa huo mnamo mwaka wa 2013, na tangu wakati huo amekuwa akikumbwa na matatizo mbalimbali ya kiafya.



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*