![Sato2109heartadvice-1320x792.jpg](https://informationcentre.co.ke/wp-content/uploads/2025/02/Sato2109heartadvice-1320x792-678x381.jpg)
Wiki iliyopita rafiki wa mpenzi wangu alinipata katika maskani ya burudani usiku. Tulilewa sana na tulipolala kwake akachovya asali. Ninajuta na nafikiria kumwambia mpenzi wangu. Nishauri.
Sasa umejua kuwa huwezi kumwamini rafiki ya mpenzi wako. Pia umejua kuwa ulevi ni hatari. Utaharibu mambo zaidi ukimwambia mpenzi wako. Atafikiria ulikuwa mpango wenu na atakuacha.
Namzidi mchumba na miaka 10, je niolewe naye?
Kwako shangazi. Nimependana na mwanamume ambaye nimemzidi umri kwa miaka 10. Niko tayari kuwa mke wake lakini yeye hajaamua. Nahofia jamaa zake watapinga kwa sababu ya umri wangu na pia nina mtoto. Nishauri.
Umri si hoja palipo na mapenzi. Tatizo ni kuwa huenda mpenzi wako hana nia ya kukuoa na inawezekana pia wazazi wake wamemshauri dhidi ya jambo hilo. Kama hayuko tayari usimlazimishe.
Aliyenipa mimba, akaruka, anataka niwe mke wa pili
Kwako shangazi. Mpenzi wangu aliniacha baada ya kunipa mimba na hatimaye akaoa mwanamke mwingine. Amekuwa akiniomba niwe mkewe wa pili lakini sitaki. Nataka kumshawishi amuache aliye naye kisha anioe. Kuna makosa?
Hali kwamba mwanamume huyo anaungama mapenzi yako kwako haina maana kuwa hampendi aliye naye. Ombi lake kuwa uwe mkewe wa pili ni ishara kuwa hataki kumuacha. Usimharibie mwenzako, tafute wako.
Hanitimizii mahitaji yangu ya pesa, natamani wa hela
Kwako shangazi. Nina mpenzi lakini mahitaji yangu ya pesa yanamshinda. Nafikiria kutafuta mwingine wa kunifaa kwa njia hiyo tu. Lakini pia naogopa kwa kuwa mpenzi wangu akijua ataniacha. Nishauri.
Unakosea kumtegemea mpenzi wako kwa mahitaji yako ya pesa. Itabidi uchague kati ya mapenzi na pesa. Kama kweli unampenda, hufai kuwa na uhusiano wa pembeni kwa manufaa ya pesa. Mapenzi ya pesa yana wenyewe na unawajua.
Leave a Reply