DAR ES SALAAM, Tanzania
RAIS Samia Suluhu Hassan amethibitisha Jumatatu, Januari 20, 2025 kwamba kuna mkurupuko wa maradhi ya Marburg, akisema kisa kimoja kimethibitishwa kufikia sasa.
“Vipimo vya maabara vilivyofanywa Kagera na baadaye kuthibitishwa jijini Dar es Salaam vimetambua mtu mmoja ameambukizwa virusi hivyo vya Marburg,” akasema kwenye mkutano na waandishi wa habari uliohudhuriwa na Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani, WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus jijini Dodoma.
Leave a Reply