Wanafunzi waliojiunga na sekondari 2021, Covid-19 ilipokuwa inatesa – Taifa Leo


WAZIRI wa Elimu, Julius Ogamba atatangaza matokeo ya Mtihani wa Kitaifa Kidato cha Nne (KCSE) 2024, leo, Alhamisi, Januari 9, 2025.

Hafla ya kutangazwa kwa matokeo hayo inaendelea katika Makao Makuu ya Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC), Jijini Nairobi.

Jumla ya watahiniwa 965, 512 waliandika mtihani huo mwaka uliopita, 2024.

Aidha, watahiniwa hao ni wanafunzi waliojiunga na shule ya Sekondari 2021 janga la Covid-19 lilipokuwa linatesa taifa na ulimwengu.

WHO, hata hivyo, baadaye ilithibitisha ulimwengu kuwa huru dhidi ya ugonjwa huo hatari uliosababisha maafa ya maelfu ya watu.

Afisa Mkuu Mtendaji KNEC, Bw David Njegere amesema matokeo ya KCSE 2024 yameandikisha historia ya kipekee nchini ikizingatiwa kuwa watahiniwa hao walijiunga na kidato cha kwanza wakati ambapo kalenda ya masomo ilikuwa imesambaratishwa na virusi vya corona.

“Kundi hili, ambalo lilianza safari ya kujiandaa kuandika KCSE Machi 2021, lilionyesha ustahimilivu na uwezo wa kuhimili mabadiliko katika kipindi kigumu kwenye mfumo wetu wa elimu,” Bw Njegere akasema, akihutubu katika makao makuu ya KNEC.

Akilinganisha idadi ya watahiniwa walioandika KCSE 2024 na 2023, afisa huyo alisema mwaka uliopita uliandikisha nyongeza ya asilimia 7.19.

“Mara ya mwisho tuliona ongezeko kama hili ilikuwa mwaka wa 2020,” Njegere akasema.

 

 

 



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*