Wanaume wawili wananitaka na nimeshindwa kuchagua, nishauri – Taifa Leo


KUNA wanaume wawili wananipigania kila mmoja akidai mimi ni mpenzi wake. Ukweli ni kuwa ni marafiki tu na sijaamua nani kati yao atakuwa mpenzi wangu. Nifanye nini?

Ni wewe tu unayeweza kumaliza ugomvi huo kwa kuwaambia ukweli. Waite uwaeleze hakuna kati yao unayemtaka kimapenzi na kwamba wakiendelea kukupigania hata huo urafiki utauvunja.

Nimemkosea vibaya dadangu kula fuska na mumewe

Nina miaka 26, naishi mjini na dada yangu ambaye ameolewa. Mwezi uliopita alisafiri kwa wiki moja. Sijui ilikuwaje mimi na mumewe tukafanya tuliyofanya. Ninajuta na nafikiria kumwambia.

Mlifanya mkijua, tena kwa maelewano. Usijaribu kumwambia dadako kwa sababu mtakosana na unaweza hata kuvunja ndoa yao. Majuto unayopitia ndiyo adhabu ya makosa yako.

Jembe limeingia kutu, ni uzee?

Mimi ni mwanamume wa miaka 52. Naishi na mke wangu pekee kwani watoto wetu ni watu wazima wako makwao. Huu ni mwaka wa pili wa kibaridi chumbani. Hiyo ni kawaida?

Naona umri umezidi na hilo huandamana na kupungua kwa ashiki. Ninaamini mlifurahia mlipokuwa na uwezo kwa hivyo si jambo la kuzua hofu, bora tu hakuna anayelalamika.

Ex ameanza za ovyo kutishia demu wangu

Nilizaa na mwanadada aliyekuwa mpenzi wangu lakini tukaachana, ingawa ninamsaidia kulea. Sijui alitoa wapi namba ya simu ya mpenzi wangu kwani ameanza kumtumia jumbe za matusi na vitisho. Nifanyeje?

Mama ya mtoto wako anafaa kushukuru kwamba unawajibikia malezi ya mtoto wenu. Huwezi kumpenda kwa lazima. Unafaa kumuonya kwa ukali kwamba asipoacha matusi utakatiza msaada huo.



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*