Watalii wawili raia wa Uholanzi wafariki dunia katika ajali Pwani – Taifa Leo


WATALII wawili walifariki dunia baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la Maji ya Chumvi huko Mariakani.

Ajali hiyo iliyotokea Jumatano saa moja asubuhi, ilihusisha gari ya kuwasafirisha watalii na gari mpya ya kusafirisha mizigo.

Kwa mujibu wa Afisa Mkuu wa trafiki ukanda wa Pwani George Kashmir, waliofariki ni raia wawili wa Uholanzi wanaume, waliokuwa wametoka Diani na wake zao.

“Ni ukweli kumetokea ajali ambayo imewauawa wanaume wawili ambao walikuwa nchini kwa likizo. Walikuwa na wake zao ambao walipata majeraha katika ajali hiyo. Aliyekuwa akiwaongoza wakati wa ziara hiyo hakuumia sana,” akasema Bw Kashmir.

Dereva wa gari hilo, wanawake hao wawili na afisa wa kuwaongoza watalii aliye katika gari hiyo walikimbizwa katika hospitali ya Mariakani kupata matibabu.



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*