Watatu wafariki, 44 wajeruhiwa katika ajali ya basi   – Taifa Leo


MSIBA ulitokea Jumamosi asubuhi wakati basi moja lilipoanguka katika eneo la Nukiat kando ya barabara ya Londiani-Muhoroni, na kusababisha vifo vya watu wawili wazima na mtoto mmoja.

Abiria wengine 44 walipata majeraha mabaya.

Kulingana na Selina Chirchir, Afisa wa Utekelezaji wa Udhibiti wa Trafiki Kaunti ya Kericho (CTEO), basi hilo lilikuwa likisafiri kutoka Mombasa kuelekea Busia kupitia barabara ya Londiani.

Inasemekana kuwa dereva alishindwa kumudu usukani na kusababisha gari hilo kuacha njia na kuanguka.

Wakati huo huo, abiria waliojeruhiwa wanapokea matibabu katika hospitali ya kaunti ndogo ya Londiani.

Miili ya marehemu ilipelekwa katika mochari ya hospitali ya Londiani

Dereva wa basi hilo alikamatwa eneo la tukio na kusindikizwa hospitalini kwa uchunguzi  wa kiafya na baadaye akazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Londiani.



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*