Watu huuguza sio kuunguza majeraha – Taifa Leo


TAREHE 20 Novemba 2024, mwanamume mmoja katika mtaa wa Pumwani jijini Nairobi alijitoma katika makazi yake yaliyokuwa yakiteketea ili kuwanusuru wanawe.

Ingawa mwanamume huyo na wanawe hawakunusurika, kitendo hicho kiliakisi hali halisi ya kujitoa mhanga. Mtu hujitoa mhanga anapokalifika nafsi, kugharimika au kuumia ilimradi wengine wanufaike.

Sina hakika iwapo kauli ‘wahanga wa ajali’, ‘wahanga wa mafuriko’ na ‘wahanga wa mkasa wa bomu’ – zilizozoeleka sana katika vyombo vya habari – huakisi miktadha ya matumizi.

Mtu huitwa ‘mhanga’ katika mazingira gani?

Hili ni swali ambalo nitalijibu katika makala tofauti.

Ni katika mkasa huo wa moto ambapo chombo fulani cha habari kiliandika habari zifuatazo: *Watu sita wameaga dunia na wengine wanaendelea kuunguza majeraha.

Kabla sijaeleza kwa nini taarifa tuliyoitaja inapotosha kisemantiki, ningependa kutaja kuwa licha ya athari ya matamshi, maneno ungua na ugua yanapotumika sawia – kama katika mkasa wa moto wa Pumwani – ni rahisi kukosewa kimatumizi.

Unguza ni kauli ya kutendesha ya kitenzi ‘ungua’ chenye maana ya kuteketea kwa moto. Kwa hivyo, kuunguza ni kuteketeza kwa moto.

Kutokana na kitenzi ‘ugua’ chenye maana ya kuwa mgonjwa – japo baadhi ya watumizi wa lugha ya Kiswahili husema *gonjeka – huzaliwa kitenzi cha kauli ya kutendesha ‘uguza’.

Ninakumbuka mmoja wa wanafunzi wangu akiniuliza kwa nini si sahihi kusema kuwa ‘kuuguza’ ni kufanya mtu kuwa mgonjwa!



Source link

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*