![Wetangula.jpg](https://informationcentre.co.ke/wp-content/uploads/2025/02/Wetangula-678x381.jpg)
SPIKA wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula ametangaza muungano wa Kenya Kwanza kuwa ulio na wabunge 165 dhidi ya 154 wa Azimio la Umoja One Kenya..
Haya yanajiri siku chache baada ya Mahakama Kuu kuamua kwamba tangazo la Bw Wetang’ula kwamba Muungano wa Kenya Kwanza ndio una wabunge wengi lilikuwa kinyume na katiba.
Uamuzi huo wa mahakama ulikuwa pigo kwa muungano wa Rais William Ruto.
Majaji watatu – John Chigiti, Lawrence Mugambi na Jairus Ngaah waliamua kuwa Bw wetang’ula alikiuka Katiba kwa kufanya uamuzi huo bila msingi wa kutosha wa kisheria.
Kwenye taarifa kwa wabunge, Spika Wetang’ula alishikilia uamuzi wake akisema mahakama haikutangaza ni muungano upi ulio wa wengi na ulio wa wachache.
Habari zaidi kufuata..
Leave a Reply