MAKAMU wa Rais nchini Ghana Mahamudu Bawumia amekubali kushindwama katika uchaguzi uliofanyika Jumamosi, Desemba 7, 2024 na kumpongeza rais wa zamani John Mahama kwa ushindi.
“Wananchi wamepiga kura na ni wazi wanataka mabadiliko,” akasema Bawumia.
Uchaguzi huo unajiri huku taifa hilo likizongwa na matatizo makubwa ya kiuchumi ambayo yalisababisha nchi hiyo kushindwa kulipa madeni yake.
Licha ya Bawumia kusalimu amri mapema, hakuna matokeo rasmi ambayo yametangazwa na Tume ya Uchaguzi.
Habari zaidi ni kadiri tunavyozipokea….
Leave a Reply